TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    Tunawapatia huduma na twatumai wote watapona- Dkt. wa Ebola DRC Jul 29, 2026
    Show notes

    Kulingana na ripoti mpya kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mlipuko wa sasa wa Ebola ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umekuwa mmoja wa milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Huko Bunia, jimboni Ituri ambako ni kitovu cha mlipuko wa sasa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakiwemo madaktari wanaongeza juhudi zao za kuwahudumia wagonjwa wakati huu ambapo ripoti zinasema watu zaidi ya 500 wamepona Ebola ya sasa. wanajamii ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo. Priscilla Lecomte aliyeko kwenye timu ya Mratibu Mkuu wa Ebola wa Umoja wa Mataifa, Julien Harneis, amezungumza na mmoja wa madaktari.


    29 JULAI 2026 Jul 29, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya wa UN, juhudi za mashirika mbalimbali za kuhamazisha wananchi DRC kuhusu udhibiti wa Ebola, na mafunzo ya STEM viziwani Zanzibar zinazolenga kuimarisha kilimo cha mwani..

    1. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na upigaji kura usio rasmi kesho Alhamisi wenye lengo la kutathmini uungwaji mkono wa wagombea saba waliojitokeza kumrithi Katibu Mkuu wa sasa Antonio Guterres anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu. Je ni nini kinafanyika? Assumpta Massoi amekuwa anafuatilia mchakato huu na nimezungumza naye angalau atupatie kwa muhtasari.
    2. Kulingana na ripoti mpya kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mlipuko wa sasa wa Ebola ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umekuwa mmoja wa milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Huko Bunia, jimboni Ituri ambako ni kitovu cha mlipuko wa sasa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakiwemo madaktari wanaongeza juhudi zao za kuwahudumia wagonjwa wakati huu ambapo ripoti zinasema watu zaidi ya 500 wamepona Ebola ya sasa. wanajamii ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.
    3. Je, ingekuwaje kama kila kijana kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania angeweza kugeuza zao la mwani kuwa suluhisho la kiuchumi la kesho yake? Hilo ndilo lengo mradi wa shirika la kiraia la ProjeKt Inspire kupitia programu yake ya Girls in STEM, au Wasichana kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ufadhili wa Canada. Kupitia warsha wa siku tatu ya masomo ya STEM, wanafunzi wamejifunza kutumia masomo hayo kuongeza thamani ya zao la mwani na kuendeleza Uchumi wa buluu.

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!


    Mafunzo ya STEM yawezesha vijana Zanzibar kuongeza thamani ya zao la mwani Jul 29, 2026
    Show notes

    Je, ingekuwaje kama kila kijana kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania angeweza kugeuza zao la mwani kuwa suluhisho la kiuchumi la kesho yake? Hilo ndilo lengo mradi wa shirika la kiraia la ProjeKt Inspire kupitia programu yake ya Girls in STEM, au Wasichana kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ufadhili wa Canada. Kupitia warsha wa siku tatu ya masomo ya STEM, wanafunzi wamejifunza kutumia masomo hayo kuongeza thamani ya zao la mwani na kuendeleza Uchumi wa buluu. Feissal Kirwa na taarifa zaidi.


    28 JULAI 2026 Jul 28, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Kuna msemo wa kiswahili usemao tahadhari kabla ya hatari na hivyo ndivyo ilivyo kwa ugonjwa wa Homa ya Ini ambapo kama mtu ataenda kufanya uchunguzi mapema anaweza kupata chanjo au matibabu, lakini kama atachelewa basi anaweza kupata hata ugonjwa wa saratani.

    Ikiwa leo ni siku ya Kimataifa ya kuelimisha kuhusu ugonjwa huo Leah Mushi wa Idhaa hii amezungumza na Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Mfumo wa Chakula na ini kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, nchini Tanzania Dkt. Swaleh Kitabu Pazi, mazungumzo yaliyofanikishwa na Evarist Mapesa Afisa Uhusiano kutoka Hospitali hiyo ya Muhimbili.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Leo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuongeza kwa kiwango kikubwa upimaji na matibabu ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi, likionya kuwa ugonjwa huo unaofahamika kwa lugha ya kiingereza na kitabibu kama Hepatitis unaweza kuua watu wengi zaidi kuliko malaria, kifua kikuu na Virusi Vya Ukimwi kwa pamoja kufikia mwaka 2040 ikiwa mwenendo wa sasa wa maambukizi utaendelea..
    2. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi zote wanachama kuhuisha dhamira yao ya kutekeleza Mkataba wa Wakimbizi wa mwaka 1951, akisema haki ya watu wanaokimbia mateso kutafuta hifadhi inazidi kutiliwa shaka, kuwekewa vikwazo au kunyimwa.
    3. Na baada ya jana ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na dawa za kulevya na uhalifu UNODC kuonesha jinsi biashara ya utapeli mtandaoni inavyozidi kukua duniani, leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limefafanua zaidi kuwa nyuma ya biashara hiyo kuna maelfu ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu wanaolazimishwa kufanya uhalifu kwa vitisho na ukatili.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!


    27 JULAI 2026 Jul 27, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza simulizi za wananchi kuhusu uhamazishaji wa kudhibiti Ebola. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC, imeonya kuhusu ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu unaofanyika kupitia matangazo bandia ya mitadaoni ya fursa za ajira. Zaidi ya watu 300,000 wanakadiriwa kushikiliwa katika vituo vya ulaghai Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, ambako hunyang’anywa hati za kusafiria na kulazimishwa kufanya utapeli mtandaoni.
    2. Kamanda wa Kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, Luteni Jenerali Ulisses De Mesquita Gomes, amethibitisha dhamira ya ujumbe huo ya kuimarisha usalama wa vituo vya afya katika eneo la Mongbwalu, jimboni Ituri, ambalo ni kitovu cha mlipuko wa Ebola. Amesema mashambulizi ya makundi yenye silaha na watu kuyakimbia makazi yao vinaweza kuvuruga ufuatiliaji wa wagonjwa na upatikanaji wa matibabu. Walinda amani wa Nepal wanaendelea kulinda raia na miundombinu ya afya, kwa kushirikiana na jeshi la Congo na mamlaka za eneo hilo.
    3. Na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC, imeonya kuhusu ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu unaofanyika kupitia matangazo bandia ya ajira mtandaoni. Zaidi ya watu 300,000 wanakadiriwa kushikiliwa katika vituo vya ulaghai Kusini-Mashariki mwa barani Asia, ambako hunyang’anywa pasipoti na kulazimishwa kufanya utapeli mtandaoni. UNODC inasema uhalifu huo sasa unasambaa hadi Afrika na maeneo mengine duniani, na kuwataka wanaotafuta ajira nje ya nchi kuthibitisha kampuni, mikataba na mawakala kabla ya kusafiri.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!


    24 JULAI 2026 Jul 24, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani kwa Maendeleo Endelevu awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kupitia Ofisi ya Rais inayohusika na Maendeleo ya Vijana, limeendelea kutumia mafunzo ya ufundi stadi kama njia ya kudumisha amani na kuwajengea uwezo vijana kiuchumi.

    Hii ni katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiwemo namba moja la kuondokana na umaskini na namba 16 linalolenga pamoja na mambo mengine kujenga amani kwenye jamii.Rashid Malekela, balozi kijana wa UNDP Tanzania alihudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Wanawake, UN Women, limeonya kuwa wanawake na wasichana katika mji wa El Obeid nchini Sudan sasa wanakabiliwa na hatari mbili wanapokwenda kuchota maji ambayo ni mashambulizi ya droni mchana yanawalazimu kusubiri hadi usiku, ambako hukumbana na ubakaji na ukatili mwingine wa kingono.
    2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema kuwa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 130,000 nchini Burundi, wengi wao wakitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRc unaweza kusitishwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu endapo halitapata ufadhili wa haraka.
    3. Na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO, umefanikiwa kurejesha utulivu katika eneo la Nyakunde jimboni Ituri, hatua iliyowezesha kurejea kwa harakati dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!


    23 JULAI 2026 Jul 23, 2026
    Show notes

    Mada kwa kina hii inakupeleka Pwani ya Kenya katika Kaunti ya Kilifi ambako mradi wa ‘Tushauriane Tuimarishe Kilimo Biashara’ unaotekelezwa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, umewezesha wakulima wa eneo hilo kubadili mtazamo na kufanya kazi kwa pamoja. Ingawa changamoto za kijinsia zimekuwepo kwa muda mrefu, sasa mradi huo umefungua njia inayoleta nuru katika uhusiano wa kijinsia, mienendo ya kaya na matokeo ya kilimo biashara. Je nini kinafanyika? Feissal Kirwa kupitia video iliyoandaliwa na FAO anakusimulia zaidi.


    Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.” Jul 22, 2026
    Show notes

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”


    22 JULAI 2026 Jul 22, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Huko DRC madini ya kimkakati mashariki mwa nchi yamekuwa kichocheo cha mizozo. Mgeni wetu leo pamoja na mambo mengine anaangazia jinsi vita imezuia wao kuendelea na uchimbaji madini.

    Yeye anaishi Goma, lakini Salama Machaano, wa redio washirika wetu, Adventista World Radio, Tumaini Mkuu iliyoko Bukavu, jimboni Kivu Kusini alifnga safari hadi Goma kuzungumza naye.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu “Utawala wa rasilimali za asili: Msingi wa amani, usalama na ustawi” chini ya kipengele cha ajenda ya “Kudumisha amani na usalama wa kimataifa.” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao hicho ameeleza vipaumbele vinne kuwa ni kuhakikisha manufaa ya haki yanapatikana kutokana na rasilimali za asili, kuimarisha uwazi na ushirikiano ili kukabiliana na biashara haramu, kukuza utatuzi wa amani wa migogoro inayohusiana na rasilimali, na kuzingatia masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika kuzuia migogoro na kujenga amani.
    2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetoa wito wa kulindwa kwa raia na kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu kuwafikia wenye uhitaji nchini Sudan baada ya shambulio lililotekelezwa juzi tarehe 20 Julai kwa kutumia ndege zisizo na rubani likilenga soko la Ar Rahad katika jimbo la Kordofan Kaskazini na kusababisha vifo vya watoto wawili na kuwajeruhi wengine sita.
    3. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kusikitishwa sana na taarifa kwamba makumi ya wahamiaji wamefariki dunia au hawajulikani walipo kufuatia kuzama kwa meli katika pwani ya Mauritania, ambapo tarehe 18 Julai manusura 38 waliokolewa na Walinzi wa Pwani wa Mauritania karibu na mji wa Nouadhibou walipokuwa wakijaribu bahati yao kuelekea nchini Hispania. IOM kupitia Mkurugenzi wake wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Sylvia Ekra, imesema watu wanaendelea kuhatarisha maisha yao kwa sababu zinazowasukuma kuondoka katika nchi zao bado zipo.
    4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!


    21 JULAI 2026 Jul 21, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Jana katika moja ya viunga vya jiji la Nairobi, wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na raia wa Afrika Kusini na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Kenya, ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela walikitembelea Kituo cha Kulelea Watoto ya Yatima kinachofahamika kwa jina Serah’s Vision Children’s Home na walikaa kituoni hapo kwa dakika 67.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Ikiwa ni miezi tisa tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas, hali ya usalama kwa raia wa Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel inaendelea kuzorota. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imesema hii leo kuwa hakuna eneo linaloweza kuchukuliwa kuwa salama kwa Wapalestina, huku Wizara ya Afya ya Palestina ikiripoti kuwa zaidi ya watu 1,100 wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel tangu Oktoba mwaka 2025.
    2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limeonya kuhusu hatari ya safari za baharini kuelekea barani Ulaya kupitia bahari ya Atlantiki baada ya watu 144 kuripotiwa kufariki au kutoweka katika pwani ya Mauritania wiki iliyopita. Katika tukio la hivi karibuni watu 387 waliokolewa katika operesheni za uokoaji.
    3. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO linasema licha ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola wa virusi aina ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuendelea kuenea kwa kasi, baadhi ya maeneo yanaanza kuonesha dalili za hali kutengamaa kutokana na hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huo.

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!


    Previous 1 6 7 8 9 10 Next

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    Bad With Money With Gabe Dunn

    6

    Bad With Money With Gabe Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights