TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    06 AGOSTI 2026 Aug 06, 2026
    Show notes

    Leo tunaangazia hatua kubwa katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi, VVU, ambapo Zimbabwe imekuwa miongoni mwa nchi za kwanza duniani kuanza kutoa Lenacapavir, sindano ya kinga inayotolewa mara mbili tu kwa mwaka na yenye ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU. Hatua hiyo inaimarisha juhudi za nchi hiyo yenye kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.2, ikilenga zaidi

    makundi yaliyo hatarini, hususan wasichana balehe na wanawake vijana ambao wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa maambukizi. Hata hivyo, pamoja na matumaini hayo, changamoto za upatikanaji wa dawa hiyo, gharama, unyanyapaa pamoja na ufikiaji wa huduma katika maeneo ya vijijini bado zinaendelea kuathiri kasi ya mafanikio. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI, UNAIDS, Feissal Kirwa wa idhaa hii amefuatilia kwa kina.


    JIFUNZE KISWAHILI - NENO MZIO Aug 06, 2026
    Show notes

    Sasa umewadia wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "MZIO"


    05 AGOSTI 2026 Aug 05, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Feissal Kirwa akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya amani na usalama, usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama, haki za binadamu na hali ya hewa.

    MUHTASARI1. Wimbi jipya la mashambulizi makubwa ya Urusi dhidi ya Ukraine yaliyosababisha vifo vya raia na majeruhi wengi, limelaaniwa vikali na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, akisisitiza kuwa raia lazima walindwe kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.Mashambulizi hayo ya usiku yaliyoanza mwezi huu wa Agosti yamekuja baada ya mwezi Julai kuwa mwezi ulioshuhudia idadi kubwa zaidi ya vifo vya raia nchini Ukraine tangu Aprili mwaka 2022. 2. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, kupitia msemaji wake Jeremy Laurence, ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa utekelezaji wa hukumu za kifo nchini Iran. Kwa mujibu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, adhabu ya kifo inaendelea kutumiwa kama njia ya kuwatia hofu wananchi na kukandamiza sauti za wanaopinga serikali.Akizungumza leo jijini Geneva, Uswisi, Jeremy Laurence amesema,“tunazihimiza mamlaka za Iran kusitisha mara moja utekelezaji wa hukumu zote za kifo na kuelekea katika kufuta kabisa adhabu ya kifo.” 3. Utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaonesha kuwa uimarikaji wa mwenendo wa hali ya hewa ya El Niño unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula duniani hadi mwaka 2027. Shirika hilo linaongeza juhudi za kujiandaa na kukabiliana na athari hizo, huku El Niño ikiwa tayari imeanza kuwaathiri watu walio katika maeneo yenye hali ya njaa. MADA KWA KINA

    Kituo kipya cha kutoa huduma kwa walioambukizwa ugonjwa wa Ebola, kinafunguliwa wiki hii huko Bunia, jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibuvyo. Kituo hiki kitakuwa kituo kikubwa zaidi nchini humo cha kutibu Ebola. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anatupitisha kwa kutumia video iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA.


    04 AGOSTI 2026 Aug 04, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama pamoja na afya.

    Muhtasari wa habari:
    1. Utapiamlo mkali nchini Afghanistan umefikia viwango vya kutisha, huku majimbo 12 yakirekodi kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa cha utapiamlo miongoni mwa watoto wakati huu watu milioni 14 wakikabiliwa na njaa kali, imesema WFP.
    2. Mjumbe Maalum wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) kwa ajili ya Sudan, Derk Segaar, leo amewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kwamba wiki iliyopita alisafiri kwa njia ya Barabara nchini Sudan na kwamba ingawa macho ya dunia yameelekezwa zaidi katika maeneo ya Darfur na Kordofan, athari za vita zinaendelea kote nchini Sudan ambayo ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani, lakini pia ni miongoni mwa migogoro inayopuuzwa zaidi.
    3. Na Umoja wa Mataifa na wadau wake wanaendelea kuisaidia Rwanda kujiandaa dhidi ya Ebola. Hatua hizo zinajumuisha ufuatiliaji katika vituo vya afya, jamii na mipakani, huku zaidi ya wahudumu 100 wakipelekwa kwenye vituo vya kuingilia nchini. Pia, wahudumu karibu 400 wanapatiwa mafunzo ya utambuzi wa mapema.
    Mada kwa kina:

    Na sasa ni wasaa wa mada kwa kina inayotupeleka nchini Afrika Kusini, ambako dawa mpya ya kujikinga na Virusi Vya Ukimwi, VVU, iitwayo Lenacapavir, imeanza kutolewa kama sehemu ya jitihada dhidi ya maambukizi mapya, hasa miongoni mwa vijana walio katika hatari kubwa zaidi.

    Kwa mara ya kwanza, mtu anaweza kujikinga na VVU, kwa kudungwa sindano moja tu kila baada ya miezi sita, bila kumeza kidonge kila siku. Lenacapavir imeonesha ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi, na sasa imeanza kutolewa katika nchi tisa barani Afrika, ikiwemo Afrika Kusini, nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani ya watu wanaoishi na VVU. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi, UNAIDS, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anakusimulia. Kwako Feissal.


    JIFUNZE KISWAHILI - NENO : KUROA Aug 03, 2026
    Show notes

    Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakwenda Burundi, ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika na mchambuzi wetu ni Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUROWA”.

    Hiki ni kitenzi kikimaanisha kuvua samaki na nomino yake ni mroaji.

    Sentensi: Mroaji ameenda ziwa Tanganyika kuangalia iwapo atapata kitoweo cha samaki.

    Hii inamaana mroaji pia ni mvuvi, na mchambuzi wetu anasema kwa ukanda wa Maziwa Makuu, mroaji ni mvuvi.


    03 AGOSTI 2026 Aug 03, 2026
    Show notes

    Ili kufahamu ni kwa namna gani Chuo Kikuu cha Mount Kenya kinawasaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kifedha lakini wana uwezo wa kitaaluma ikiwa ni sehemu ya juhudi za chuo hicho kushiriki katika kuhimiza Malengo 17 ya maendeleo endelevu,SDG na kuunga mkono utekelezaji wake., Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye alikiwakilisha chuo hicho katika Kongamano la Kimataifa kuhusu Elimu ya Juu lililofanyika mwezi uliopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani


    31 JULAI 2026 Jul 31, 2026
    Show notes

    Hii leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya, katika Kijiji cha Embulbul kilichoko Kaunti ya Kajiado, ambako Shirika lisilo la kiserikali la Tulivu Safe Haven, lililoanzishwa kwa kushirikiana na wadau wakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa, linatekeleza hatua mbalimbali za kuwasaidia wanawake.

    Hii ni pamoja na kuwaokoa na kuwahifadhi manusura wa ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia makazi salama, ushauri nasaha, msaada wa kisheria na uwezeshaji wa kiuchumi, sambamba na kuwarejesha shuleni wasichana walionusurika. Je, nini kinafanyika? Kupitia video iliyoandaliwa na Redio washirika wetu Domus, Feissal Kirwa amefuatilia simulizi za manusura na kutuandalia makala hii.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Maabara tembezi ya kupima virusi vya Ebola imewekwa katika mji wa mpakani wa Kasenyi ulioko kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kuna hatari kubwa ya kushamiri kwa mlipuko wa Ebola kutokana na harakati nyingi za safari. Dkt. Olga Ntumba kutoka WHO ambayo inafadhili maabara hiyo inayotoa majibu ndani ya saa moja, amesema “virusi haviheshimu mipaka. Maabara hii ina mchango muhimu kubaini mapema wagonjwa, kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa, kubadilishana taarifa na juhudi za mwitikio kwenye ukanda mzima.”
    2. Mioto ya nyika ikiendelea kutikisa maeneo ya kaskazini mwa dunia shirika la Umoja wa Matiafa la Afya duniani, WHO limekumbusha kuwa moshi utokanao na mioto hiyo ya nyika huvuka taifa, kanda na hata mabara na kuwa na madhara kwa watu hata wanaoishi mbali na moto wenyewe. Hivyo limetangaza mambo tisa ya kuzingatiwa ikiwemo kusikiliza taarifa za mamlaka kama vile viwango vya uchafuzi wa hewa, kuvaa barakoa na kusalia ndani ya nyumba na kufunga madirisha iwapo hujashauriwa kuhama.
    3. Na wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama ikianza kesho Agosti Mosi, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake, lile la afya, (WHO) na la kuhudumia watoto, (UNICEF) umetaka nchi kuimarisha mifumo ya afya ili iweze kupatia akina mama na watoto wachanga msaada wa kufanikisha unyonyeshaji bora ambao ni msingi wa ukuaji bora wa mtoto na afya ya mama anayenyonyesha. Halikadhalika utekelezaji wa kanuni ya kimataifa kuhusu matangazo ya bidhaa za mbadala wa maziwa ya mama.

    Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, karibu!


    Jifunze Kiswahili: Maana ya neno, “KUSOROZA.” Jul 30, 2026
    Show notes

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUSOROZA.”


    30 JULAI 2026 Jul 30, 2026
    Show notes

    Hii leo tunakuletea mada kwa kina. Mlipuko wa sasa wa ebola ya virusi vya Bundibugyo uliotangazwa rasmi huko DRC mwezi Mei mwaka huu unazidi kuongezeka kwa kasi isiyo ya kawaida, wamesema maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa wakizungumza na waandishi wa habari Karl Skau, Kaimu Mkuu wa WFP, na ndio tunakupeleka nchini humo kufuatilia juhudi za kuudhibiti.

    1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ni wakati wa dunia kuungana kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji wa watu, hususan aina mpya inayokua kwa kasi ya kulazimishwa kufanya utapeli kwa njia ya mtandao. Katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Watu inayoadhimishwa kila mwaka tarehe thelathini Julai, amesema wahalifu wanawavutia watu kwa ahadi za ajira nzuri, lakini baadaye wanawafanya mateka na kuwalazimisha kuendesha utapeli mtandaoni. Guterres amezitaka nchi kuridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Uhalifu wa Mtandao uliopitishwa mwaka 2024, kushirikiana kuvunja mitandao ya uhalifu na kuwasaidia manusura kurejea katika maisha yao ya kawaida.
    2. Nchini Ukraine, mashambulizi makubwa ya usiku yaliyojumuisha makombora na mamia ya ndege zisizo na rubani yamesababisha vifo na majeruhi katika maeneo kadhaa ya makazi, yakiwemo miji ya Kryvyi Rih, Kyiv na Lviv. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, imesema nyumba na shule za awali zimeharibiwa huku watoto wakiwa miongoni mwa waliouawa na kujeruhiwa. Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limesema watoto watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, huku likiendelea kutoa msaada wa dharura wa kisaikolojia na usaidizi wa kifedha kwa familia zilizoathirika.
    3. Na Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, amelaani hatua za serikali ya Uganda zinazodaiwa kuendelea kubana uhuru wa msingi na kuzima sauti za wanaokosoa serikali. Amesema tangu uchaguzi mkuu wa Januari mwaka huu, viongozi wa upinzani, wanaharakati wa haki za binadamu na waandishi wa habari wamekumbwa na vitendo vya kutoweshwa, kukamatwa kiholela na mateso. Kupitia taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Bwana Türk ni kwamba ofisi hiyo imepokea taarifa zinazoonesha kuongezeka kwa ushiriki wa jeshi katika kutekeleza majukumu ambayo kwa kawaida hufanywa na taasisi za kiraia. Aidha, baadhi ya vyombo vya habari vimelazimika kusitisha shughuli zake kwa muda.
    4. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na leo tunamkaribisha Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUSOROZA. ”

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!


    Mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa kuingia ng’we nyingine kesho Jul 29, 2026
    Show notes

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakuwa na upigaji kura usio rasmi kesho Alhamisi wenye lengo la kutathmini uungwaji mkono wa wagombea saba waliojitokeza kumrithi Katibu Mkuu wa sasa Antonio Guterres anayemaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu. Je ni nini kinafanyika? Assumpta Massoi amekuwa anafuatilia mchakato huu na nimezungumza naye angalau atupatie kwa muhtasari.


    Previous 1 5 6 7 8 9 10 Next

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    Bad With Money With Gabe Dunn

    6

    Bad With Money With Gabe Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights