Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina nayomulika mabaharia wanawake, ambapo tunamsikia mmoja wao, Mary Jane Siy Chuan, Fundi wa Umeme melini, akisema, “ninapoingia melini, wafanyakazi wengine wanahoji kama vile, kwa nini kuna mwanamke baharini.”Kukiwa na dalili za kuwa sitisho la mapigano kati ya Iran na Israel linaanza kushika mizizi, mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA Rafael Grossi. ametoa wito kwa Iran kuanza tena ushirikiano na jumuiya ya kimataifa ili kupunguza mvutano unaoendelea kuhusu mpango wake wa nyuklia. Grossi amesema amempa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ombi la kukutana na kushirikiana, “akitilia mkazo kuwa hatua hii inaweza kufungua njia ya suluhisho la kidiplomasia kwa mgogoro wa muda mrefu” kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.Msemaji wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) Thameen Al-Kheetan ameripoti leo kwamba hadi kufikia sasa takribani Wapalestina 410 wameuawa na jeshi la Israeli wakati wakijaribu kupata msaada kutoka kwa vituo vipya vya misaada vilivyokumbwa na utata huko Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limeripoti leo kuwa linakadiria kuwa wakimbizi milioni 2.5 duniani kote watahitaji kuhamishiwa Kwenda katika nchi nyingine mwaka ujao.Na mashianani fursa ni yake Zahra Nader, raia wa Afghanistan ambaye ni mwandishi wa habari na mwanaharakati wa haki za wanawake, anayeishi uhamishoni kutokana na zahma nchini mwake. Akizungumza kutoka Geneva, USwisi anasimulia hali halisi ya wanawake nchini Afghanistan, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia haki zao..Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!