TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    25 SEPTEMBA 2026 Sep 25, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo unafanyika mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu maandalizi dhidi ya majanga ya milipuko ya magonjwa na kama nilivyokudokeza kuwa tutakuwa na maoni na ushauri wa baadhi ya wananchi wa Afrika Mashariki kwa viongozi wanaoshiriki mkutano huo, tunaanzia nchini Uganda, kisha tuelekee nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo linafanya Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Kuzuia, Kujiandaa na Kukabiliana na Magonjwa ya Milipuko, unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kupitisha tamko la kisiasa kuhusu maandalizi na mwitikio wa magonjwa ya milipuko. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Antonio Guterres, Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed amesema dunia inahitaji mshikamano, usawa na hatua madhubuti za kimataifa ili kutomwacha mtu yeyote nyuma na kujifunza kutokana na uzoefu wa hivi karibuni akisema “Janga la COVID-19 lilitufundisha kwamba, katika dunia yetu iliyounganishwa, hakuna nchi inayoweza kujilinda yenyewe. Tulijifunza jambo hili kwa gharama kubwa sana ya kibinadamu na kiuchumi.”
    2. Tukielekea Afrika, Hama hama ya watu kutokana na mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, inmelilazimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, kuongeza ufuatiliaji wa Ebola katika mipaka, vituo vya wakimbizi na njia za usafiri. Hadi Septemba 21, zaidi ya watu 7,700 walikuwa wamethibitishwa kuwa na Ebola, huku 3,700 wakifariki.
    3. Na nchini Yemen takriban watoto milioni 2.2 wenye umri wa chini ya miaka 5 wanakumbwa na utapiamlo kila uchao hawajui pa kula wala pa kulala kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF likisistiza kuwa usalama ndio kipaumbele ili watoto hao waweze kuishi kama Watoto. Akizungumza Geneva Uswisi kwa njia ya video kutoka Aden, Yemen Mwakilishi wa UNICEF nchini humo, Akhil Iyer, amesema “Tunashuhudia ongezeko la utapiamlo mkali mtoto 1 kati ya 4 anautapiamlo mkali na Watoto 200 wako katika hali mbaya sana ya unyafuzi.”

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    24 SEPTEMBA 2026 Sep 24, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. “Kuwa mkimbizi si chaguo wala hiyari ni shuruti inayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa amani sababu ya vita na kila mtu anaweza kuwa mkimbizi siku moja.”

    Hiyo ni kauli ya Marry Nyiriak Maker Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii kandoni mwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu wakati wa maadhimisho ya miaka 75 ya mkataba wa wakimbizi. Mary anatanabaisha safari yake kutoka Sudan hadi kambi ya wakimbizi ya Kakuma Kenya na hatimaye hapa Marekani.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    23 SEPTEMBA 2026 Sep 23, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho Septemba 24 viongozi wa dunia wanaokutana hapa New York, Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa watakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ongezeko la kina cha maji ya bahari duniani.

    Hatimaye wanatarajiwa kupitisha azimio la kusaidia mataifa yanayokumbwa na madhara yatokanayo na ongezeko hilo. Kutoka Nairobi, Kenya, Assumpta Massoi kwa ushirikiano na Radio washirika wetu Pangani FM ya mkoani Tanga, mashariki mwa Tanzania na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, nchini humo, UNIC, anamulika madhara ya ongezeko la kina cha maji ya Bahari ya Hindi, kilichosababisha maji hayo kuingia ndani ya Mto wa Pangani. Sasa wakulima na wavuvi wanahaha.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema kuwa maendeleo, haki za binadamu na amani ni nguzo zinazopaswa kusonga mbele kwa pamoja ili kuleta ustawi wa watu wote duniani. Ametoa kauli hiyo mjini New York, Marekani, wakati wa Mkutano wa Ngazi ya Juu uliofanyika kuadhimisha miaka 40 tangu kupitishwa kwa Azimio la Haki ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa la mwaka 1986. Amesisitiza akisema, “maadhimisho haya ni zaidi ya wakati wa kutafakari. Ni wito wa kuchukua hatua, kutimiza ahadi ya kulinda haki ya maendeleo kwa wote. Kupanua ushiriki na ujumuishi wa watu na nchi katika maendeleo ya dunia. Na kusukuma mbele zaidi maendeleo.”
    2. Tukisalia na suala hilo, mmoja wa vijana kutoka barani Afrika, nchini Cameroon, Nakita Aboya ni miongoni mwa watu wanaohudhuria mikutano ya kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA81. Anasema ingawa hakupata nafasi ya kushiriki katika Mkutano huu wa leo wa Ngazi ya Juu uliofanyika kuadhimisha miaka 40 tangu kupitishwa kwa Azimio la Haki ya Maendeleo la Umoja wa Mataifa la mwaka 1986 lakini ana maoni akisema, “Ndiyo, ninaamini kwamba kila mtu ana haki ya maendeleo, mradi tu maendeleo hayo hayakiuki haki za wengine. Ninaamini kila mtu ana haki ya maendeleo. Lakini ujumbe mmoja tu kwa viongozi; tekelezeni ahadi zenu. Kwa mfano, mara nyingi katika hotuba tunasikia kauli kama: Vijana ndio msingi; inabidi vijana wajumuishwe; ooh hatuwezi kufanya chochote bila vijana; vijana, vijana, vijana. Lakini zaidi ya maneno hayo, ni hatua gani zinazochukuliwa? Kwa hiyo, ujumbe mmoja ninaoweza kutoa ni: asante sana kwa ahadi zenu, lakini tafadhali sasa tekelezeni ahadi hizo.”
    3. Na hotuba za viongozi katika Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zinaendelea leo ikiwa ni siku ya pili. Rais wa Ndaishimiye wa Burundi ameutumia mkutano huu kusisitiza nafasi ya Afrika duniani,..anasema “Burundi, ikiwa inashikilia Uenyekiti wa Muungano wa Afrika, imechagua umoja, mshikamano na kuchukua hatua. Tumechagua Afrika yenye amani, Afrika iliyounganishwa, Afrika inayojilisha yenyewe, Afrika inayobadilisha na kuongeza thamani ya rasilimali zake, Afrika inayowapa vijana wake fursa na uwezo wa kuunda na kubuni, Afrika inayosimamia hatima yake yenyewe. Na tunachagua mfumo wa ushirikiano wa kimataifa ulioboreshwa, ambao kila eneo, kila jamii na kila taifa linahesabiwa. Kwa Afrika, tunataka Umoja wa Mataifa wenye uwakilishi mpana zaidi, wenye ufanisi zaidi na ulio karibu zaidi na wananchi.”

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    22 SEPTEMBA 2026 Sep 22, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mabadiliko ya tabianchi hayawaathiri watu wote kwa kiwango sawa.

    Baadhi ya nchi zimejenga uchumi wao kwa miongo kadhaa kupitia matumizi makubwa ya nishati ya mafuta, huku nyingine zilizochangia kidogo katika uzalishaji wa gesi chafu zikikabiliwa na mafuriko, vimbunga, ukame, ongezeko la kina cha bahari na kupotea kwa njia za kujipatia riziki.

    Hili ndilo kiini cha mjadala kuhusu haki na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ambao utafanyika kesho Jumatano . Lakini haki hiyo ina maana gani? Nani anapaswa kubeba gharama? Na kizazi kijacho kitaachiwa dunia ya aina gani?

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefungua pazia asubuhi ya leo saa za New York, Marekani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antono Guterres kupitia hotuba yake ambayo ni ya mwisho katika tukio hili amegusa mambo mengi miongoni likiwa kuhusu ushauri wake kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya mageuzi katika Baraza la Usalama ili liakisi hali halisi ya ulimwengu wa leo na kuwa na uhalali pamoja na ufanisi unaohitajika kukabiliana na changamoto za sasa.
    2. Tuondoke hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, ambako viongozi wa ulimwengu sasa wanaendelea kutoa hotuba zao nakupeleka mashinani hususan Nairobi, Kenya kusikia vijana wanataka nini.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    Balozi Thigo: Kuwalinda watoto zama za AI na teknolojia ni muhimu sana Sep 21, 2026
    Show notes

    Kesho Jumanne tarehe 22 Septemba mbali ya kufunguliwa kwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matanfa wa UNGA81, kandoni mwa mjadala huo kutakuwa na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. Balozi Philip Thigo anayehusika na masuala ya AI kutoka Kenya ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo amenieleza kwa nini suala hili ni muhimu katika mkutano wa kesho na nini wanakitarajia


    Maandalizi ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA81 Sep 21, 2026
    Show notes

    Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataofa UNGA81 unafungua pazia kesho Jumanne ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa kwa kina na nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa ikiwemo kuwasilisha tarifa zao wenzangu Leah Mushi na Anold Kayanda waafuatilia maandalizi ya mjadala huo.


    21 SEPTEMBA 2026 Sep 21, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu na vijana kuhusu siku ya amani, ufunguzi wa UNGA81, Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni.

    1. Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali kuendeleza amani.
    2. Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataofa UNGA81 unafungua pazia kesho Jumanne ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa kwa kina na nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa ikiwemo kuwasilisha tarifa zao
    3. Kesho Jumanne tarehe 22 Septemba mbali ya kufunguliwa kwa mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Matanfa wa UNGA81, kandoni mwa mjadala huo kutakuwa na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Akili Mnemba, au Akili Unde AI, na Usalama wa watoto Mtandaoni. Balozi Philip Thigo anayehusika na masuala ya AI kutoka Kenya ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo amenieleza kwa nini suala hili ni muhimu katika mkutano wa kesho na nini wanakitarajia.

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!


    Siku ya amani duniani, vijana wapaza sauti zao Sep 21, 2026
    Show notes

    Leo ni siku ya amani duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amepongeza watu wote mashinani wakiwemo watumishi wa kujitolea, wachechemuzi na viongozi wa mashirika ya kiraia wanaojitolea kwa hali na mali kuendeleza amani.


    18 SEPTEMBA 2026 Sep 18, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo kufuatilia mapambano dhidi ya ebola ambayo yameanza kupata matumaini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.

    1. Mlipuko wa sasa wa 17 wa Ebola wa virusi vya Bundibugyo huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umegharimu zaidi wanawake na wasicha kwa kuwa wengi wao wako mstari wa mbele kuhudumia wagonjwa na familia zao licha ya hatari kubwa ya kuambukizwa. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva, Uswisi, kwa njia ya mtandao kutoka Kinshasa DRC, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, (UN Women) nchini humo, Dkt. Setcheme Mongbo, amesema. “Wanawake na wasichana huosha miili ya marehemu na kushiriki katika shughuli nyingine za mazishi, wao ndio wanaokusanya na kutoa maji na chakula kwa wanafamilia. Na suala la utoaji wa huduma hizo ni muhimu sana katika mnyororo mzima wa maambukizi linapokuja suala la Ebola.”
    2. Kumekuwa na ripoti za kushtusha za dhidi ya raia na wafungwa wa kivita wakati huu kukiwa na mashambulizi kamili ya kijeshi yanayofanywa na jeshi la Urusi huko Kyiv nchini Ukraine. Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu Shabia Mantoo amewaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo kuwa. “Zaidi ya wagonjwa 1,000 wamerekodiwa na wafanyakazi wetu wa Kamati ya wa Ufuatiliaji wa Haki za Binadamu kuanzia tarehe 24 Februari 2022 hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk ana wasiwasi mkubwa kwamba vitendo hivyo vya kuchukiza vinaendelea karibu katikati ya vurugu zisizoisha, na anahimiza vikomeshwe mara moja. Pia anatoa wito wa uchunguzi wa haraka, wa kina, na usio na upendeleo kuhusu madai yote ya unyanyasaji wa kingono, na kwa wale watakaopatikana na hatia wafikishwe mbele ya sheria.”
    3. Na, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeonya kuwa msaada wa dharura unaotolewa kupitia mfumo wake wa pamoja wa kibinadamu nchini Sudan unaweza kuisha ndani ya wiki mbili zijazo kutokana na ukosefu wa fedha. IOM inasema inahitaji dola milioni 15 kuendeleza operesheni hiyo kwa kiwango cha chini kwa miezi 12, wakati watu milioni 8.6 bado wakiwa wakimbizi wa ndani nchini Sudan.

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!


    17 SEPTEMBA 2026 Sep 17, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda nchini Kenya ambako Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kwamba taifa hilo la Afrika Mashariki litakabiliwa El Nino kuanzia mwezi ujao wa Oktoba hadi Desemba mwaka huu wa 2026.

    El Nino huweze kusababisha mvua kubwa na kwingineko ukame mkali. Kufuatia onyo hilo, tayari shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) kwa kushirikiana na serikali wameanza kuchukua hatua za mapema ili kuepusha madhara makubwa. Sasa nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii, kupitia mahojiano yaliyofanywa na Mercy Korir, mwanafunzi wa vitendo kwenye kituo cha huduma za Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya, UNIS, ameandaa mada hii kwa kina. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Dunia inaingia katika kipindi ambacho upatikanaji usiotabirika wa maji unazidi kuwa kawaida, imeonya leo ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO. Ripoti hiyo inasema mwaka 2025 ulikuwa miongoni mwa miaka yenye mtiririko mdogo zaidi wa mito katika miongo mitatu na nusu. Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo, amesema hali hiyo ni ishara inayoendelea kwa muongo mmoja. Akisistiza hilo Wayne Jenkinson, Mkurugenzi, Kitengo cha Hidrologia WMO anasema, “Mara nyingi maji hayapatikani mahali tunapoyahitaji, wala wakati tunapoyahitaji.”
    2. Zaidi ya watoto 57,000 wameyakimbia makazi yao nchini Yemen katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kutokana na mapigano mapya, huku wengine wakiuawa, kujeruhiwa au kutoweka. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF linaonya kuwa vurugu hizo zinazidisha janga la kibinadamu katika nchi ambako zaidi ya watoto milioni 12 wanategemea misaada baada ya zaidi ya muongo mmoja wa mzozo. Msemaji wa UNICE Joe English amesema watoto wengi nchini Yemen hawajui maisha mengine isipokuwa mzozo na kuhama kutoka kwenye makazi yao. Na kwamba “Hawa ni watoto ambao tayari wamepitia miaka ya njaa, kufurushwa makwao na migogoro, na sasa wanalazimishwa kuondoka tena katika makazi yao”.
    3. Na Wanawake duniani kote bado wanapata kwa wastani asilimia 20 chini ya wanaume, licha ya juhudi za muda mrefu za kukuza usawa kazini. Katika Siku ya Kimataifa ya Usawa wa Mishahara, Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Kazi Duniani (ILO) na la masuala ya Wanawake UN Women yanasema pengo hilo si jambo lisiloepukika, na yanataka hatua kuhakikisha wanawake wanalipwa sawa kwa kazi zenye thamani sawa. ILO inasema “Usawa wa mishahara ni suala la haki, kanuni, utu na usawa wa kijamii – kwa kila mfanyakazi, kila mahali” wakati UN Women ikisisitiza kuwa “Usawa wa mishahara si suala la haki pekee; unaimarisha familia, uchumi na jamii.” Mashirika hayo yanasema sasa kinachohitajika ni hatua za kubadili ahadi za usawa wa mishahara kuwa uhalisia.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    1 2 3 10 Next

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    Bad With Money With Gabe Dunn

    6

    Bad With Money With Gabe Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights