TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    Kutoka kuhofia kuhukumiwa hadi kuwa mhamasishaji wa afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya Nov 04, 2026
    Show notes

    Zipporah Achieng, mama kijana nchini Kenya, ambaye aliwahi kuhofia kuhukumiwa alipokwenda kliniki kupata huduma za afya baada ya kujifungua, sasa amegeuka kuwa mhamasishaji wa afya ya uzazi kwa vijana. Kupitia mpango wa Together for SRHR, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika manne ya Umoja wa Mataifa kwa lengo hilo la kuelimisha vijana na vijana balehe kuhusu afya ya uzazi, Zipporah anawasaidia vijana kupata taarifa sahihi na huduma za afya ya uzazi bila unyanyapaa. Augustine Aramba na taarifa zaidi.


    Mashambulizi ya droni na uhaba wa mafuta nchini Sudan vyazima matumaini ya raia wanaohitaji msaada wa dharura Nov 04, 2026
    Show notes

    Hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuwa tete huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) yakilenga miundombinu muhimu ya kiraia, ikiwemo vituo vya nishati na mafuta, kuvuruga huduma za afya na maji na kuweka hatarini maisha ya maelfu kwa maelfu ya raia. Flora Nducha anatujuza zaidi


    04 NOVEMBA 2026 Nov 04, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu, hali ya kibinadamu nchini Sudan, na juhudi za wahamasishaji na mashirika ya UN za kuhusu huduma za afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya.

    1. Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) inasema hatua sita zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu zina uwezo wa kuokoa maisha ya watu milioni 1.6 kila mwaka, huku zikizalisha manufaa ya kiuchumi yenye thamani ya matrilioni ya dola.
    2. Hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuwa tete huku mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) yakilenga miundombinu muhimu ya kiraia, ikiwemo vituo vya nishati na mafuta, kuvuruga huduma za afya na maji na kuweka hatarini maisha ya maelfu kwa maelfu ya raia.
    3. Zipporah Achieng, mama kijana nchini Kenya, ambaye aliwahi kuhofia kuhukumiwa alipokwenda kliniki kupata huduma za afya baada ya kujifungua, sasa amegeuka kuwa mhamasishaji wa afya ya uzazi kwa vijana. Kupitia mpango wa Together for SRHR, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika manne ya Umoja wa Mataifa kwa lengo hilo la kuelimisha vijana na vijana balehe kuhusu afya ya uzazi, Zipporah anawasaidia vijana kupata taarifa sahihi na huduma za afya ya uzazi bila unyanyapaa.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    WHO: Hatua sita za kiafya na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinaweza kuokoa maisha milioni 1.6 kila mwaka Nov 04, 2026
    Show notes

    Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) inasema hatua sita zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu zina uwezo wa kuokoa maisha ya watu milioni 1.6 kila mwaka, huku zikizalisha manufaa ya kiuchumi yenye thamani ya matrilioni ya dola. Anold Kayanda ameifuatilia ripoti hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.


    Wakazi wa Lui nchini Sudan Kusini wachoshwa na vita Nov 03, 2026
    Show notes

    Wakazi wa Lui, jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanalilia amani, elimu na fursa za ajira kwa vijana baada ya kuchoshwa na vita. Kilio hicho kimetolewa wakati walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, walipotembelea eneo hilo kusikiliza changamoto za wananchi kupitia kampeni ya Hear Us, Act Now for Peace yaani Tusikilize, Chukua Hatua sasa kwa ajili ya amani. Cynthia Akhangwa na taarifa zaidi.


    Jumuiya ya kimataifa yahimizwa kuisaidia Ukraine wakati huu wa msimu wa baridi Nov 03, 2026
    Show notes

    Mcheza filamu maarufu duniani Nikolaj Coster-Waldau anayefahamika zaidi kwa kuigiza katika filamu ya Game of Thrones ambaye pia ni Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo Duniani UNDP ametembelea nchini Ukraine kujionea hali ilivyo wakati huu ambao mapigano baina ya Urusi na Ukraine yakiendelea. Leah Mushi anatujuza zaidi kuhusu safari yake hiyo.


    03 NOVEMBA 2026 Nov 03, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wa DRC nchini Burundi, Msimu wa baridi kwa waathirika wa vita nchini Ukraine, na juhudi za Umoja wa Mataifan na wakazi wa Sudan kusinini za ujenzi wa amani.

    1. Takriban wakimbizi 125,000 nchini Burundi wako katika hatari ya kukosa msaada wa chakula wa kuokoa maisha kuanzia Januari mwakani, iwapo ufadhili wa dharura hautapatikana. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linasema wakimbizi wengi wamekimbia mzozo wa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakitafuta usalama na chakula. Sasa WFP inahitaji dola milioni 40 ili kuendeleza na kupanua wigo wa msaada huo.
    2. Mcheza filamu maarufu duniani Nikolaj Coaster-Waldau anayefahamika zaidi kwa kuigiza katika filamu ya Game of Thrones ambaye pia ni Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo Duniani UNDP ametembelea nchini Ukraine kujionea hali ilivyo wakati huu ambao mapigano baina ya Urusi na Ukraine yakiendelea.
    3. Wakazi wa Lui, jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanalilia amani, elimu na fursa za ajira kwa vijana baada ya kuchoshwa na vita. Kilio hicho kimetolewa wakati walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, walipotembelea eneo hilo kusikiliza changamoto za wananchi kupitia kampeni ya Hear Us, Act Now for Peace yaani Tusikilize, Chukua Hatua sasa kwa ajili ya amani.

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!


    Wakimbizi 125,000 nchini Burundi hatarini kukosa chakula kuanzia Januari 2027, WFP yaomba msaada wa dharura Nov 03, 2026
    Show notes

    Takriban wakimbizi 125,000 nchini Burundi wako katika hatari ya kukosa msaada wa chakula wa kuokoa maisha kuanzia Januari mwakani, iwapo ufadhili wa dharura hautapatikana. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linasema wakimbizi wengi wamekimbia mzozo wa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakitafuta usalama na chakula. Sasa WFP inahitaji dola milioni 40 ili kuendeleza na kupanua wigo wa msaada huo. Flora Nducha na ripoti zaidi.


    Ethiopia yaandaa mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Timu za Dharura za Matibabu Afrika Nov 02, 2026
    Show notes

    Zaidi ya washiriki 800 kutoka nchi zaidi ya 100 wanatarajiwa kukutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, katika mkutano wa kimataifa wa kujadili namna ya kuimarisha uwezo wa nchi kukabiliana na dharura za kiafya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu kwa wakati.Flora Nducha na taarifa zaidi


    Umoja wa Mataifa wataka uwajibikaji kwa mauaji kwa wanaowadhuru wanahabari Nov 02, 2026
    Show notes

    Ikiwa leo ni siku ya kukomesha kutowajibisha kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa Habari duniani hali inaonesha kuzorota na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kukomeshwa vyoto vya ukatili dhidi ya wanahabari na kuhakikisha wanaohusika na mauaji yao wanafikishwa mbele ya sheria, akieleza kuwa mauaji sita kati ya kila saba ya wanahabari duniani hayapati haki. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi


    Previous 1 2 3 4 5 19 Next

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn

    6

    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights