TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    Shule iliyokuwa ikisomesha mamia ya wanafunzi nchini Haiti sasa ni makazi ya wakimbizi wa ndani 3,000 Nov 10, 2026
    Show notes

    Shule moja katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, iliyokuwa ikipokea mamia ya wanafunzi, sasa imegeuka kuwa makazi ya muda ya takribani watu 3,000 waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu yenye silaha. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, wakazi hao wanasema maisha katika maskani hayo ni magumu, huku msaada wa kibinadamu ukiwa muhimu kwa maisha yao ya kila siku. Flora Nducha anafafanua zaidi katika taarifa hii


    10 NOVEMBA 2026 Nov 10, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia takwimu za afya barani Afrika, hali ya wakimbizi nchini Haiti, na changamoto za malezi ya watototo wenye ulemavu.

    1. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), kupitia Ofisi zake za Kanda ya Mashariki ya Mediterania na Afrika, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limeandaa Jukwaa la Kwanza la Takwimu za Afya Afrika lililoanza leo Jumanne jijini Nairobi, Kenya. Mercy Korir, mwanafunzi wa vitendo kwenye Kituo cha Habari za Umoja wa Mataifa (UNIS) jijini Nairobi, amezungumza na Daktari Hillary Kipruto ambaye ni Afisa Ufundi na Mifumo ya taarifa za Afya kwenye Ofisi ya WHO Kanda ya Afrika iliyoko Congo, Brazaville. Daktari Kipruto, pamoja na mambo mengine anaelezea umuhimu wa takwimu za afya kwani akisema hakuna maendeleo kwenye sekta ya afya bila takwimu.
    2. Shule moja katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, iliyokuwa ikipokea mamia ya wanafunzi, sasa imegeuka kuwa makazi ya muda ya takribani watu 3,000 waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu yenye silaha. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, wakazi hao wanasema maisha katika maskani hayo ni magumu, huku msaada wa kibinadamu ukiwa muhimu kwa maisha yao ya kila siku.
    3. Kulea mtoto mwenye changamoto ya kiafya kunaambatana na changamoto nyingi kwa wazazi au walezi. Mbaya zaidi ni pale juu ya changamoto nyingine, wanakumbana na changamoto kubwa zaidi ya unyanyapaa. Nchini Kenya, kupitia ufadhili na mafunzo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake, UN Women, na msaada kutoka kwa familia na jamii, wazazi wa watoto wenye mtindio wa ubongo wameweza kukabiliana na changamoto hizo.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika laanza Nairobi, Kenya Nov 10, 2026
    Show notes

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), kupitia Ofisi zake za Kanda ya Mashariki ya Mediterania na Afrika, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, limeandaa Jukwaa la Kwanza la Takwimu za Afya Afrika lililoanza leo Jumanne jijini Nairobi, Kenya. Mercy Korir, mwanafunzi wa vitendo kwenye Kituo cha Habari za Umoja wa Mataifa (UNIS) jijini Nairobi, amezungumza na Daktari Hillary Kipruto ambaye ni Afisa Ufundi na Mifumo ya taarifa za Afya kwenye Ofisi ya WHO Kanda ya Afrika iliyoko Congo, Brazaville. Daktari Kipruto anaanza kwa kuelezea umuhimu wa takwimu za afya kwani anasema hakuna maendeleo kwenye sekta ya afya bila takwimu. Akisema pillars anamaanisha nguzo.


    Wazazi wa watoto wenye mtindio wa ubongo nchini Kenya wavunja ukimya kuhusu unyanyapaa Nov 10, 2026
    Show notes

    Kulea mtoto mwenye changamoto ya kiafya kunaambatana na changamoto nyingi kwa wazazi au walezi. Mbaya zaidi ni pale juu ya changamoto nyingine, wanakumbana na changamoto kubwa zaidi ya unyanyapaa.Nchini Kenya, kupitia ufadhili na mafunzo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake, UN Women, na msaada kutoka kwa familia na jamii, wazazi wa watoto wenye mtindio wa ubongo wameweza kukabiliana na changamoto hizo. Kupitia taarifa hii inayosimuliwa na Augustine Aramba, baadhi ya wazazi wanasimulia kuhusu changamoto hizi na jinsi walivyoweza kukabiliana nazo.


    09 NOVEMBA 2026 Nov 09, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP31, umeanza leo jijini Antalya, Uturuki, ukimulika ajenda mbalimbali ikiwemo ya ufadhili wa hatua za kukabiliana na tabianchi.

    Nchini Tanzania, Shirika la Uoja wa Mataofa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa kushirikiana na serikali imetia saini makubaliano ya ruzuku ya dola milioni 2, sawa na shilingi bilioni 5.2, kusaidia taasisi za kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali 49 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Fedha hizo kutoka Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF), kupitia Mpango wa Ruzuku Ndogo (SGP), zinalenga kusaidia miradi ya uhifadhi wa mazingira, bioanuai, vyanzo vya maji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

    Pia tunakuleteamuhtasari wa habari:

    1. Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP31, umefunguliwa leo Antalya, Uturuki, kwa wito wa kuharakisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mtaifa kuhusu Tabianchi, Simon Stiell, amesema: “COP31 lazima uongeze kasi ya kutafuta na kutekeleza suluhisho.” Rais wa mkutano huo, Murat Kurum, ameonya, “Kuchelewa kuchukua hatua ni mojawapo ya gharama kubwa zaidi katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.” Naye Waziri wa Tabianchi wa Australia, Chris Bowen, ambaye ni rais wa COP31amesema, “Mabadiliko ya tabianchi yapo sasa. Si utabiri wala makisio. Ni hali halisi inayowakabili mabilioni ya watu.” Mkutano huo unajadili ufadhili, nishati safi na hatua za kuimarisha mnepo dhidi ya athari za tabianchi.
    2. Kwenye mkutano huo huo wa COP31, vijana hawakuachwa nyuma “Mimi ni Marynsia Mangu nikiwakilisha Tanzania katika majadiliano ya uhamishaji wa teknolojia kwenye COP31. Tunazungumzia kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, kujiandaa na athari za mabadiliko ya tabianchi na jinsi ambavyo nchi zinazoendelea zitapata fedha kutoka katika nchi zilizoendelea. Kwa Tanzania, hizi ni habari ambazo zinagusa uchumi na maisha ya watu. Kwa mujibu wa uchambuzi ya Benki ya Dunia, athari za mabadiliko ya tabianchi zinaweza kusukuma watu milioni mbili nukta sita zaidi kwenye umaskini nchini Tanzania kufikia mwaka 2030”.
    3. Na mwaka 2026 unaendelea kushuhudia mfululizo wa muda mrefu wa ongezeko la joto duniani, kuyeyuka kwa barafu na kupanda kwa kina cha bahari. Hali hiyo inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kutokana na tukio kali la hali ya hewa ya El Niño, ambalo linatarajiwa kuongeza joto na matukio ya hali mbaya ya hewa hadi mwaka 2027, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO) iliyotolewa leo. Ripoti hiyo inaangazia athari zinazotokana na mabadiliko hayo kwa mazingira, uchumi na maisha ya kila siku.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    06 NOVEMBA 2026 Nov 06, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Vijana huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania, mashariki mwa bara la Afrika wameshiriki mafunzo ya kuimarisha amani na kuchochea maendeleo endelevu miongoni mwa wanajamii.

    Halikadhalika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini humo kwa kushirikiana na wadau wengine wengine wa maendeleo pia yalijikita katika kuwajengea vijana hao uelewa kuhusu Afya ya Akili, usaidizi wa kisaikolojia na kijamii. Rashid Malekela wa UNDP Tanzania amehudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina, kuelekee visiwani Zanzibar kumsikiliza

    Pia tunakuleteamuhtasari wa habari:

    1. Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya Uhamiaji (IOM) na Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) yametoa wito wa kuongeza msaada wa kibinadamu nchini Sudan, ambako watu milioni 15.4 wanahitaji huduma za dharura za malazi, huku uhaba wa fedha ukipunguza uwezo wa kuwasaidia. Mkuu wa Ujumbe wa IOM nchini Sudan, Mohamed Refaat, amesema akiba ya misaada inaelekea kuisha. “Jana tu, tulikuwa na malori 16 yaliyowasili Darfur, lakini hayo ndiyo yalikuwa ya mwisho katika akiba yetu. Tunakabiliwa na matatizo makubwa.
    2. Sasa afya, Chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya Ebola zitaongezwa katika majaribio ya kitabibu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakati nchi hiyo ikikabiliana na mlipuko wa virusi vya Bundibugyo.
    3. Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amezitaka nchi duniani kuheshimu sheria za kimataifa na kuepuka matumizi haramu ya nguvu, akionya kuwa migogoro, ukosefu wa usawa na mabadiliko ya tabianchi vinatishia ushirikiano wa kimataifa. Akizungumza leo katika Chuo Kikuu cha Salamanca nchini Hispania, Guterres ametaja migogoro ya Ukraine, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Gaza na Yemen, akisisitiza umuhimu wa diplomasia na ulinzi wa raia. Ameonya pia kuwa matumizi ya fedha nyingi za kijeshi huku misaada ya kibinadamu na maendeleo ikipungua yanaongeza changamoto duniani.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    Wanawake nchini Uganda wako mstari wa mbele kutatua migogoro na kujenga amani Nov 05, 2026
    Show notes

    Matumizi ya pombe, ukatili wa kijinsia na migogoro ya kijamii ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha amani katika baadhi ya maeneo nchini Uganda. Hata hivyo, wanawake wamekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu, huku zaidi ya wapatanishi 1,500 wakipatiwa mafunzo ya kuzuia migogoro na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women kabla haijaongezeka. Augustine Aramba na taarifa zaidi.


    Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu - UNICEF Nov 05, 2026
    Show notes

    Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu kati ya mwaka 2021 na 2025, yakihatarisha maisha ya mamilioni ya watu, hususan watoto. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, linasema hali hiyo inawaweka watoto katika hatari ya magonjwa, utapiamlo na ukatili. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anatupa maelezo zaidi.


    05 NOVEMBA 2026 Nov 05, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia athari za vita kwa upatikanaji wa maji, Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami, na Juhud iza wanawake nchini Uganda za kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa amani..

    1. Mashambulizi dhidi ya mifumo ya maji katika maeneo yenye migogoro yameongezeka mara tatu kati ya mwaka 2021 na 2025, yakihatarisha maisha ya mamilioni ya watu, hususan watoto. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, linasema hali hiyo inawaweka watoto katika hatari ya magonjwa, utapiamlo na ukatili.
    2. Hii leo ni Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami. Binafsi kwa ufupi ninaweza kukweleza kuwa Tsunami ni msururu wa mawimbi makubwa yanayotokana na mtikisiko wa maji chini ya Bahari lakini Kamal Kishore, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kupunguza Hatari za Maafa ambaye pia ni Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa au majanga (UNDRR) katika kuadhimisha siku hii, ameeleza hatua tatu muhimu ambazo ukizichukua zinaweza kukuokoa dhidi ya tsunami. Anold Kayanda anatusaidia kueleza kwa lugha ya Kiswahili
    3. Matumizi ya pombe, ukatili wa kijinsia na migogoro ya kijamii ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha amani katika baadhi ya maeneo nchini Uganda. Hata hivyo, wanawake wamekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu, huku zaidi ya wapatanishi 1,500 wakipatiwa mafunzo ya kuzuia migogoro na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women kabla haijaongezeka.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    UNDRR: Ukikumbwa na Tsunami, hatua hizi zitakusaidia kunusurika Nov 05, 2026
    Show notes

    Kama nilivyokudokeza hapo awali, hii leo ni Siku ya Kimtaifa ya Kukuza Uelewa Kuhusu Tsunami. Binafsi kwa ufupi ninaweza kukweleza kuwa Tsunami ni msururu wa mawimbi makubwa yanayotokana na mtikisiko wa maji chini ya Bahari lakini Kamal Kishore, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kupunguza Hatari za Maafa ambaye pia ni Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa au majanga (UNDRR) katika kuadhimisha siku hii, ameeleza hatua tatu muhimu ambazo ukizichukua zinaweza kukuokoa dhidi ya tsunami. Anold Kayanda anatusaidia kueleza kwa lugha ya Kiswahili.


    Previous 1 2 3 4 19 Next

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn

    6

    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights