TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    02 NOVEMBA 2026 Nov 02, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kukomesha kutowajibisha kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa Habari, mifumo ya kukabiliana na dharura za kiafya barani Afrika, na uhamasishaji wa uchunguzi wa mapema ya saratani ya matiti nchini Kenya.

    1. Ikiwa leo ni siku ya kukomesha kutowajibisha kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa Habari duniani hali inaonesha kuzorota na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kukomeshwa vyoto vya ukatili dhidi ya wanahabari na kuhakikisha wanaohusika na mauaji yao wanafikishwa mbele ya sheria, akieleza kuwa mauaji sita kati ya kila saba ya wanahabari duniani hayapati haki.
    2. Zaidi ya washiriki 800 kutoka nchi zaidi ya 100 wamekusanyika Addis Ababa Ethiopia kujadili namna ya kuimarisha mifumo ya kukabiliana na dharura za kiafya na kuboresha upatikanaji wa huduma za matibabu zinazookoa maisha.
    3. Je, unajua kuwa unaweza kutumia dakika chache tu kujichunguza matiti yako ukiwa nyumbani? Oktoba ni mwezi wa kimataifa wa kuelimisha umma kuhusu saratani ya matiti na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasisitiza umuhimu wa kutambua dalili, kujichunguza na kupata matibabu kwa wakati. Nchini Kenya, Asha Akinyi Olum kutoka kaunti ya Bungoma ni miongoni mwa wanawake waliofikiwa na huduma za uchunguzi kupitia mpango unaoungwa mkono na WHO.

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!


    Kujichunguza matiti kwa dakika chache kunaweza kuokoa maisha - WHO Nov 02, 2026
    Show notes

    Je, unajua kuwa unaweza kutumia dakika chache tu kujichunguza matiti yako ukiwa nyumbani? Oktoba ni mwezi wa kimataifa wa kuelimisha umma kuhusu saratani ya matiti na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasisitiza umuhimu wa kutambua dalili, kujichunguza na kupata matibabu kwa wakati. Nchini Kenya, Asha Akinyi Olum kutoka kaunti ya Bungoma ni miongoni mwa wanawake waliofikiwa na huduma za uchunguzi kupitia mpango unaoungwa mkono na WHO. Tupate taarifa Zaidi kutoka kwa Cynthia Akhangwa.


    30 OKTOBA 2026 Oct 30, 2026
    Show notes

    Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa hii leo ambapo utasikia muhtasari wa habari na kisha mada kwa kina kutoka Nairobi nchini Kenya ambapo washindi wawili wa tuzo ya Umoja wa Mataifa wamezungumza.


    Siku ya Kimataifa ya huduma na usaidizi - ILO yataka uwekezaji katika uchumi wa huduma Oct 29, 2026
    Show notes

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO, limetaka hatua za haraka kuchukuliwa kuboresha huduma za malezi na uangalizi, pamoja na mazingira ya kazi kwa watu wanaotoa huduma hizo, likionya kuwa upungufu wa huduma bora unaweza kuongeza ukosefu wa usawa wa kijinsia. Wito huo umetolewa wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Huduma na Usaidizi, leo tarehe 29 Oktoba. Flora Nducha na taarifa zaidi


    UNICEF Tanzania yaimarisha lishe ya watoto kupitia Jiko Darasa Makete Oct 29, 2026
    Show notes

    Nchini Tanzania, katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe, mradi wa Lishe ya Mwanao unaowezeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF chini ya ufadhili wa Norway umeasaidia kupunguza tatizo la uzito mdogo na udumavu kwa watoto kupitia mafunzo ya upishi wa vyakula vyenye virutubisho vinavyopatikana katika jamii. Augustine Aramba na taarifa zaidi.


    29 OKTOBA 2026 Oct 29, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Huduma na Usaidizi, haki za binadamunchini Sudan, na lishe bora kwa watoto kwa lengo la kutokomeza udumavu nchini Tanzania.

    1. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO, limetaka hatua za haraka kuchukuliwa kuboresha huduma za malezi na uangalizi, pamoja na mazingira ya kazi kwa watu wanaotoa huduma hizo, likionya kuwa upungufu wa huduma bora unaweza kuongeza ukosefu wa usawa wa kijinsia. Wito huo umetolewa wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Huduma na Usaidizi, leo tarehe 29 Oktoba.
    2. Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ukatili dhidi ya raia katika maeneo yenye migogoro duniani, hususan Sudan, ambako mauaji, ubakaji na mashambulizi yanayotumia ndege zisizo na rubani yanaendelea kugharimu maisha ya watu. Aidha amepongeza vijana kwa kusimama kidete kudai haki na uwajibikaji.
    3. Nchini Tanzania, katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe, mradi wa Lishe ya Mwanao unaowezeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF chini ya ufadhili wa Norway umesaidia kupunguza tatizo la uzito mdogo na udumavu kwa watoto kupitia mafunzo ya upishi wa vyakula vyenye virutubisho vinavyopatikana katika jamii.

    Mwenyeji wako ni Cynthia Akhangwa, karibu!


    Türk aonya kuhusu ukatili dhidi ya raia katika migogoro yanayoendelea duniani Oct 29, 2026
    Show notes

    Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ukatili dhidi ya raia katika maeneo yenye migogoro duniani, hususan Sudan, ambako mauaji, ubakaji na mashambulizi yanayotumia ndege zisizo na rubani yanaendelea kugharimu maisha ya watu. Aidha amepongeza vijana kwa kusimama kidete kudai haki na uwajibikaji. Leah Mushi ana taarifa zaidi.


    Jifunze Kiswahili: Maana ya neno, Mgao au Mwaego Oct 28, 2026
    Show notes

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo tunamkaribisha NTAHOMBAYE HUSSEIN, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, Mgao au Mwaego.


    28 OKTOBA 2026 Oct 28, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina. Huko DRC ambako mlipuko wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo bado unaendelea, ufuatiliaji wa wagonjwa waliopona ni muhimu kama moja ya sehemu za mwitikio dhidi ya mlipuko wa ugonjwa huo uliothibitishwa mwezi Mei mwaka huu, ukiwa ni mlipuko wa 17.

    Wagonjwa waliopona, mara baada ya kuruhusiwa kwenye vituo vya matibabu, (ETC), huendelea kupatiwa misaada ikiwemo ya kisaikolojia na uchunguzi kupitia kliniki mahsusi.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili:

    1. Ripoti mpya ya jarida la kisayansi la Lancet, kwa kushirikiana na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani, WHO, imeonya kuwa mwaka 2023, takribani watu 710,000 walifariki dunia kutokana na joto kali, ikiwa ni rekodi ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa. Zaidi ya asilimia 70 ya vifo hivyo vimehusishwa na mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli za binadamu.
    2. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linaendelea kujadili wanawake, amani na usalama, huku ripoti ya Katibu Mkuu ikionesha kuwa wanawake na wasichana walikuwa robo ya raia zaidi ya 37,000 waliouawa katika migogoro ya kivita mwaka jana. Ripoti hiyo inaonya pia kuhusu ongezeko la ukatili wa kingono na kutengwa kwa wanawake katika mazungumzo ya amani.
    3. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limeonya kuhusu kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu eneo la Moyale, mpakani mwa Kenya na Ethiopia, baada ya mapigano upande wa Ethiopia kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbilia Kenya kutafuta usalama.
    4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo tunamkaribisha NTAHOMBAYE HUSSEIN, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, Mgao au Mwaego.

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!


    27 OKTOBA 2026 Oct 27, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina ambayo ni muendelezo wa mazungumzo ya Leah Mushi wa Idhaa hii na Dokta Theophilus Wangata, Mkurugenzi Mtendaji wa Housepital kampuni inayotoa huduma za kitabibu majumbani huko nchini Kenya.

    Hapo jana alieleza walengwa wakubwa ni pamoja na wagonjwa waliotoka hospitalini, wenye maumivu, wenye magonjwa sugu, pia alieleza watoa huduma wanaofanya nao kazi. Na sasa nakurejesha tena kwa Leah akiendelea na mahojiano.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari:

    1. Katika masuala ya afya Dkt. Meg Doherty, Kiongozi wa kiufundi wa majaribio ya chanjo kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO amesema jaribio ya chanjo ya Ervebo dhidi ya Ebola ya virusi vya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC litajibu maswali muhimu ya kisayansi kuhusu namna ya kudhibiti mlipuko wa sasa wa 17 na kujiandaa kwa milipuko ijayo. Amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, kwamba, “kwa sasa, muundo wa jaribio umeandaliwa ili kuwawezesha watu wanaokidhi vigezo kupokea chanjo kati ya siku moja na siku 21 baada ya kuwa katika hatari ya kuambukizwa.”.
    2. Kwa mazingira ambapo wahenga walinena mchezo kwao hutunzwa na ndivyo ilivyokuwa leo hapa Nairobi Kenya wakati Ofisi za Umoja wa Mataifa zilipatia tuzo vijana wawili wanaotekeleza kwa vitendo Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, SDGs ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 81 ya Umoja huo. Mshindi wa kwaza ni Dkt. Bornface Otieno Owino mkulima mbunifu aliyeweka kando udaktari na kuingia kwenye kilino bunifu kinachoinua maisha ya jamii yake..
    3. Na tukislaia na washindi wa Tuzo hili, mshindi wa pili ni mwanamazingira Kevin Wekesa anayetumia michezo kulinda mazingira ambapo baada ya kupokea tuzo anatoa ujumbe wake.

    Mwenyeji wako ni Cynthia Akhangwa, karibu!


    Previous 1 2 3 4 5 6 19 Next

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn

    6

    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights