Show notes
Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
-Harakati za kutokomeza Ebola ya virusi vya Bundibugyo huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, zinakumbwa na mkwamo kwani wananchi wamesema wanahitaji sio tu matibabu dhidi ya ugonjwa huo, bali pia maji, chakula, matibabu ya malaria, chanjo na huduma za afya uzazi, mama na mtoto.
-hirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mpya kuhusu ubora wa maji ya kunywa, likizitaka nchi kuimarisha kanuni, ufuatiliaji na usimamizi wa hatari zozote zinazoweza kujitokeza . Licha ya maendeleo yaliyopatikana, watu bilioni 2.1 bado hawana huduma ya maji ya kunywa inayosimamiwa kwa usalama
-kingo wa Magharibi eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, OHCHR, imezisihi mamlaka za Israel kusaidia familia za Wapalestina ambazo zimezingirwa na walowezi ndani ya nyumba zao kwa siku kadhaa, huku kampeni ya kuwapokonya ardhi yao ikizidi kushika kasi.
-Na katika mada kwa kina leo tunajikita na Akili Mnemba (AI) na kilimo na kilimo biashara Afrika utamsikia Afisa wa FAO Meshack Malo