TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    17 SEPTEMBA 2026 Sep 17, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda nchini Kenya ambako Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imetoa tahadhari ya kwamba taifa hilo la Afrika Mashariki litakabiliwa El Nino kuanzia mwezi ujao wa Oktoba hadi Desemba mwaka huu wa 2026.

    El Nino huweze kusababisha mvua kubwa na kwingineko ukame mkali. Kufuatia onyo hilo, tayari shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) kwa kushirikiana na serikali wameanza kuchukua hatua za mapema ili kuepusha madhara makubwa. Sasa nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii, kupitia mahojiano yaliyofanywa na Mercy Korir, mwanafunzi wa vitendo kwenye kituo cha huduma za Habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya, UNIS, ameandaa mada hii kwa kina. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Dunia inaingia katika kipindi ambacho upatikanaji usiotabirika wa maji unazidi kuwa kawaida, imeonya leo ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO. Ripoti hiyo inasema mwaka 2025 ulikuwa miongoni mwa miaka yenye mtiririko mdogo zaidi wa mito katika miongo mitatu na nusu. Katibu Mkuu wa WMO, Celeste Saulo, amesema hali hiyo ni ishara inayoendelea kwa muongo mmoja. Akisistiza hilo Wayne Jenkinson, Mkurugenzi, Kitengo cha Hidrologia WMO anasema, “Mara nyingi maji hayapatikani mahali tunapoyahitaji, wala wakati tunapoyahitaji.”
    2. Zaidi ya watoto 57,000 wameyakimbia makazi yao nchini Yemen katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kutokana na mapigano mapya, huku wengine wakiuawa, kujeruhiwa au kutoweka. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF linaonya kuwa vurugu hizo zinazidisha janga la kibinadamu katika nchi ambako zaidi ya watoto milioni 12 wanategemea misaada baada ya zaidi ya muongo mmoja wa mzozo. Msemaji wa UNICE Joe English amesema watoto wengi nchini Yemen hawajui maisha mengine isipokuwa mzozo na kuhama kutoka kwenye makazi yao. Na kwamba “Hawa ni watoto ambao tayari wamepitia miaka ya njaa, kufurushwa makwao na migogoro, na sasa wanalazimishwa kuondoka tena katika makazi yao”.
    3. Na Wanawake duniani kote bado wanapata kwa wastani asilimia 20 chini ya wanaume, licha ya juhudi za muda mrefu za kukuza usawa kazini. Katika Siku ya Kimataifa ya Usawa wa Mishahara, Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Kazi Duniani (ILO) na la masuala ya Wanawake UN Women yanasema pengo hilo si jambo lisiloepukika, na yanataka hatua kuhakikisha wanawake wanalipwa sawa kwa kazi zenye thamani sawa. ILO inasema “Usawa wa mishahara ni suala la haki, kanuni, utu na usawa wa kijamii – kwa kila mfanyakazi, kila mahali” wakati UN Women ikisisitiza kuwa “Usawa wa mishahara si suala la haki pekee; unaimarisha familia, uchumi na jamii.” Mashirika hayo yanasema sasa kinachohitajika ni hatua za kubadili ahadi za usawa wa mishahara kuwa uhalisia.

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    Burundi yazindua chanjo dhidi ya HPV kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 Sep 16, 2026
    Show notes

    Hivi karibuni, Burundi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, pamoja na wadau wengine, imezindua mpango wa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, H mpango unaolenga kuwachanja wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi 14. Anold Kayanda na taarifa zaidi.


    Jengo la makazi laporomoka Gaza, takribani watu 100 wahofiwa kunaswa chini ya vifusi Sep 16, 2026
    Show notes

    Hofu na majonzi vimetanda Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 100, wakiwemo watoto 50, walikuwa wakiishi katika jengo hilo wakati lilipoanguka. Operesheni za uokoaji zinaendelea, huku Umoja wa Mataifa ukisema kila dakika ni muhimu katika kujaribu kuokoa maisha. Flora Nducha na taarifa zaidi


    16 SEPTEMBA 2026 Sep 16, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia uokoaji Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi, ushirikiano na Umoja wa Mataifa, na chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi nchini Burundi.

    1. Hofu na majonzi vimetanda Gaza baada ya jengo moja kuporomoka na kuwanasa watu chini ya vifusi. Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 100, wakiwemo watoto 50, walikuwa wakiishi katika jengo hilo wakati lilipoanguka. Operesheni za uokoaji zinaendelea, huku Umoja wa Mataifa ukisema kila dakika ni muhimu katika kujaribu kuokoa maisha.
    2. Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuhusu kuongezeka kwa vitisho, kulipiza visasi na ufuatiliaji wa kidijitali unaovuka mipaka dhidi ya watu na wadau yanayoshirikiana na mfumo wake unaohusiana na masuala ya haki za binadamu. Kufahamu kwa kina kilichomo kwenye ripoti hyo nimezungumza na Selina Jerobon ambaye amefuatilia kwa kina.
    3. Hivi karibuni, Burundi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, pamoja na wadau wengine, imezindua mpango wa chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, mpango unaolenga kuwachanja wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi 14

    Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!


    Ukandamizaji unaovuka mipaka na vitisho dhidi ya washirika wake wa masuala ya haki za binadamu Sep 16, 2026
    Show notes

    Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuhusu kuongezeka kwa vitisho, kulipiza visasi na ufuatiliaji wa kidijitali unaovuka mipaka dhidi ya watu na wadau yanayoshirikiana na mfumo wake unaohusiana na masuala ya haki za binadamu. Kufahamu kwa kina kilichomo kwenye ripoti hyo nimezungumza na Selina Jerobon ambaye amefuatilia kwa kina. Selina Jerobon anaeleza zaidi.


    15 SEPTEMBA 2026 Sep 15, 2026
    Show notes

    Hii leo tunakuletea mada kwa Kina ambayo leo inaangazia jinsi huduma za afya ya msingi zinavyosogezwa karibu na wananchi katika Kaunti ya Nairobi nchini Kenya. Kupitia msaada wa UNICEF. Pia tunakuletea muhtasari wa habazi kama zifuatazo.

    1. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2026 kuhusu Hatari za Dunia imebainisha kuwa hofu kuhusu uwezekano wa kutokea kwa vita vikubwa duniani imeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na sasa vita hivyo vinatajwa kuwa miongoni mwa hatari kubwa na za haraka zaidi zinazoikabili dunia. Ripoti hiyo, iliyokusanya maoni ya watu 1,300 kutoka serikalini, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia, sekta binafsi na wanazuoni, inaonesha kuwa vita vikubwa vimepanda kwa nafasi 16 katika orodha ya vitisho vinavyoweza kutokea hivi karibuni.
    2. Umoja wa Mataifa unasema kuwa ufadhili wa kina unahitajika hivi sasa ili kuhakikisha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) unadhibitiwa kwani kasi ya kusambaa ni kubwa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, Dkt. Olivier le Polain ambaye ni Mkuu wa Idara ya Hatua dhidi ya Magonjwa na Uchambuzi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) amesema “huko jimboni Kivu Kaskazini, tunaona idadi ya wagonjwa inaongezeka. Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, idadi ya wagonjwa kwa wiki imeongezeka kutoka wagonjwa 100 hadi 200, kwa wiki iliyopita. Kwa hiyo ni ongezeko la mara mbili la wagonjwa katika kipindi cha wiki chache tu huko Kivu Kaskazini.”.
    3. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amemteua mwanadiplomasia wa Kenya Martin Kimani kuwa Mkuu wa Masuala ya Afrika kwenye Idara inayohusika na Masuala ya Kisiasa na Ujenzi wa Amani pamoja na Operesheni za Amani za Umoja wa Mataifa. Taarifa hiyo ya uteuzi imetolewa jijini New York, Marekani na Msemaji wa Umoja wa Mataifa. Kimani ana uzoefu wa miaka 25 katika uhusiano wa kimataifa, amani na usalama, pamoja na diplomasia ya kimataifa. Aliwahi kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa jijini New York kuanzia 2020 hadi 2024. Wakati Kenya ilipokuwa mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2021–2022, Balozi Kimani aliwahi kuwa Rais wa Baraza hilo mwezi Oktoba 2021. Pia aliongoza Kikosi Kazi kuhusu kuzuia na kutatua migogoro barani Afrika.

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!


    IAEA yaangazia hali ya nyuklia Syria, na wasiwasi kuhusu Iran na Ukraine Sep 14, 2026
    Show notes

    Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limesema maendeleo yamepatikana katika kutatua masuala yaliyosalia kuhusu ukaguzi wa nyuklia nchini Syria, huku wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ukiendelea kuwa wa dharura. Anold Kayanda amefuatilia kwa kina taarifa hiyo na kuandaa taarifa hii.


    Mlo shuleni wabadilisha maisha ya Dieudo na familia yake nchini DR Congo Sep 14, 2026
    Show notes

    Kwa watoto wengi, chakula shuleni si mlo tu, bali ni fursa ya kuhudhuria masomo, kujifunza na kuwa na matumaini ya kutimiza ndoto zao. Huko Kananga, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mwanafunzi Dieudo mwenye umri wa miaka 11 ni mfano thabiti wa jinsi njaa ilivyokuwa ikiathiri wanafunzi kabla ya kuanzishwa kwa mpango wa mlo shuleni unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. Leah Mushi anasimulia zaidi.


    14 SEPTEMBA 2026 Sep 14, 2026
    Show notes

    Hii leo tunaangazia masuala ya mpango wa nyuklia mashariki ya kati, mlo shuleni nchini DR Congo, na ukosefu wa ajira kwa wanafunzi baada ya kuhitimu masomo ya vyuo vikuu Turkana nchini Kenya.

    1. Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limesema maendeleo yamepatikana katika kutatua masuala yaliyosalia kuhusu ukaguzi wa nyuklia nchini Syria, huku wasiwasi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ukiendelea kuwa wa dharura.
    2. Kwa watoto wengi, chakula shuleni si mlo tu, bali ni fursa ya kuhudhuria masomo, kujifunza na kuwa na matumaini ya kutimiza ndoto zao. Huko Kananga, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mwanafunzi Dieudo mwenye umri wa miaka 11 ni mfano thabiti wa jinsi njaa ilivyokuwa ikiathiri wanafunzi kabla ya kuanzishwa kwa mpango wa mlo shuleni unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP.
    3. Duniani kote hivi sasa vijana wanapomaliza masomo hujikuta hawana cha kufanya kwani matarajio ya kupata ajira ili kuanza kujipatia kipato huyeyuka na hivyo kusalia katika sintofahamu. Vivyo hivyo kwa kijana mmoja wa kike huko kaunti ya Turkana nchini Kenya ambaye ndoto zilitwama lakini ujio wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP ulileta tena nuru katika maisha yake.

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!


    Ukosefu wa ajira baada ya masomo katika kaunti ya Turkana, Kenya, waelekeza vijana kwenye kilimo Sep 14, 2026
    Show notes

    Duniani kote hivi sasa vijana wanapomaliza masomo hujikuta hawana cha kufanya kwani matarajio ya kupata ajira ili kuanza kujipatia kipato huyeyuka na hivyo kusalia katika sintofahamu. Vivyo hivyo kwa kijana mmoja wa kike huko kaunti ya Turkana nchini Kenya ambaye ndoto zilitwama lakini ujio wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP ulileta tena nuru katika maisha yake. Assumpta Massoi kutoka Nairobi, Kenya anasimulia zaidi.


    Previous 1 8 9 10 11 12 19 Next

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn

    6

    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights