TopPodcast.com
Menu
  • Home
  • Top Charts
  • Top Networks
  • Top Apps
  • Top Independents
  • Top Podfluencers
  • Top Picks
    • Top Business Podcasts
    • Top True Crime Podcasts
    • Top Finance Podcasts
    • Top Comedy Podcasts
    • Top Music Podcasts
    • Top Womens Podcasts
    • Top Kids Podcasts
    • Top Sports Podcasts
    • Top News Podcasts
    • Top Tech Podcasts
    • Top Crypto Podcasts
    • Top Entrepreneurial Podcasts
    • Top Fantasy Sports Podcasts
    • Top Political Podcasts
    • Top Science Podcasts
    • Top Self Help Podcasts
    • Top Sports Betting Podcasts
    • Top Stocks Podcasts
  • Podcast News
  • About Us
  • Podcast Advertising
  • Contact
Not in our directory?
Add Show Here
Podcast Equipment
Center

toppodcastlogoOur TOPPODCAST Picks

  • Comedy
  • Crypto
  • Sports
  • News
  • Politics
  • True Crime
  • Business
  • Finance

Follow Us

toppodcastlogoStay Connected

    View Top 200 Chart
    Back to Rankings Page
    Business

    Habari za UN – Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    Advertise
    • Apple Podcasts
    • Google Play
    • Spotify

    Latest Episodes:
    10 JULAI 2026 Jul 10, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania katika visiwa vya Zanzibar. Tunamulika jinsi serikali ya Zanzibar kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP wanaboresha huduma za utalii kwa kutumia Akili Mnemba au AI.

    1. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa kupunguzwa kwa misaada rasmi ya maendeleo tangu Januari 2025 kumesababisha takribani wanawake na wasichana milioni moja duniani kupoteza huduma muhimu katika nchi zilizoathiriwa na migogoro. Ikitolewa leo Geneva, Uswisi na New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN Women, ripoti hiyo iliyopatiwa jina ‘Zaidi ya Kiwango cha Kuvumilika’ miongoni mwa changamoto ilizozitaja ni pamoja na kuwa asilimia 84 ya mashirika ya wanawake yameripoti kuongezeka kwa mahitaji ya huduma, lakini takribani asilimia 90 ya mahitaji hayawezi tena kuyakidhi na kwamba mashirika mawili kati ya matano yanatarajia kufungwa ndani ya mwaka mmoja kutokana na ukosefu wa fedha.
    2. Huko Sudan, nchi inayoumia kwa vita kwa miaka minne sasa, kumetangazwa mlipuko mpya wa ugonjwa wa kipindupindu hali inayozidisha wasiwasi kuhusu usalama wa jamii zilizo hatarini, hususan katika mji wa El-Obeid uliozingirwa, ambako mashambulizi ya kila siku ya ndege zisizo na rubani yanaendelea kuzuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Dkt. Shible Sahbani, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) nchini Sudan akizungumza kwa njia ya video na waandishi wa habari leo mjini Geneva, uswisi amesema, “tumerekodi zaidi ya wagonjwa 1,330 wa kipindupindu, huku watu 114 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Hii inaonesha kiwango cha vifo miongoni mwa wagonjwa wa kipindupindu cha asilimia 13.7, ambacho ni cha juu sana. Na bila shaka, msimu wa mvua unaotarajiwa utaifanya hali kuwa mbaya zaidi.”
    3. Na utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuhusu Ufuatiliaji wa Elimu Duniani, umeonesha kuwa misaada ya kimataifa kwa sekta ya elimu imeendelea kupungua na nchi 113 duniani zinatumia fedha nyingi kulipa madeni kuliko pesa wanazoziwekeza kwenye elimu. Matokeo ya utafiti huo yamewekwa wazi leo mbele ya viongozi kutoka nchi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa Mageuzi ya Elimu TES+4 unaofanyika Paris, Ufaransa ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kwanza wa Mageuzi ya Elimu uliofanyika mwaka 2022 na pia ili kusongesha zaidi ufikiaji wa Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu linalohusu Elimu Bora.

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!


    Ushirikiano kati ya wahudumu wa afya na wanajamii unavyosaidia kupambana na Ebola DR Congo Jul 09, 2026
    Show notes

    Wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo ukiendelea kuenea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua zimepigwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Uwezo wa kutoa matibabu umeongezeka, linasema Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO na kuwaruhusu ndugu kuwaona jamaa zao kumeongeza utayari wa wagonjwa kujitokeza. Anold Kayanda na maelezo zaidi.


    09 JULAI 2026 Jul 09, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunaangazia washindi wa Tuzo ya UNFPA, harakati za kutokomeza Ebola nchini DRC, na watoto wenye ulemavu nchini Kenya.

    1. Profesa Serigne Gueye, daktari bingwa wa mfumo wa njia ya haja ndogo kutoka Senegal na mmoja wa wataalamu mashuhuri duniani wa matibabu ya fistula ya uzazi, amesema kutokomeza tatizo hilo kunategemea kuimarishwa kwa mifumo ya huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma za dharura za uzazi kwa wakati.
    2. Wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo ukiendelea kuenea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua zimepigwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Uwezo wa kutoa matibabu umeongezeka, linasema Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO na kuwaruhusu ndugu kuwaona jamaa zao kumeongeza utayari wa wagonjwa kujitokeza.
    3. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa juzi Julai 7 imeeleza kuwa ingawa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yameboresha maisha ya mabilioni ya watu duniani, kasi ya maendeleo bado haitoshi kufikia malengo yaliyowekwa ili kufikia mwaka 2030 yawe yametimizwa. Na ingawa Umoja wa Mataifa unaendelea kuhamasisha kuwa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma katika maendeleo lakini kundi la watu wenye ulemavu bado ​ linakumbana na changamoto nyingi. Kevin Keitany wa Radio washirika wetu Radio Domus ya nchini Kenya ametembelea moja ya mashirika yanayosaidia watu wenye ulemavu nchini humo ili kuangazia harakati zao za kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!


    Kila mtu anazaliwa na kipaji chake tusiwatenge wenye ulemavu – Jofreshia Family and Community Services Jul 09, 2026
    Show notes

    Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa juzi Julai 7 imeeleza kuwa ingawa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yameboresha maisha ya mabilioni ya watu duniani, kasi ya maendeleo bado haitoshi kufikia malengo yaliyowekwa ili kufikia mwaka 2030 yawe yametimizwa. Na ingawa Umoja wa Mataifa unaendelea kuhamasisha kuwa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma katika maendeleo lakini kundi la watu wenye ulemavu bado ​ linakumbana na changamoto nyingi. Kevin Keitany wa Radio washirika wetu Radio Domus ya nchini Kenya ametembelea moja ya mashirika yanayosaidia watu wenye ulemavu nchini humo ili kuangazia harakati zao za kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.


    Mshindi wa tuzo ya UNFPA aelezea linalopaswa kufanyika kutokomeza fistula ya uzazi ifikapo 2030 Jul 09, 2026
    Show notes

    Profesa Serigne Gueye, daktari bingwa wa mfumo wa njia ya haja ndogo kutoka Senegal na mmoja wa wataalamu mashuhuri duniani wa matibabu ya fistula ya uzazi, amesema kutokomeza tatizo hilo kunategemea kuimarishwa kwa mifumo ya huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma za dharura za uzazi kwa wakati. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.


    Jifunze Kiswahili: Maana za neno "KICHAKATA MATINI". Jul 08, 2026
    Show notes

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KICHAKATA MATINI".


    08 JULAI 2026 Jul 08, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho, Julai 9, ni miaka 15 tangu Sudan Kusini ipate uhuru wake kutoka Sudan. Hata hivyo, matumaini ya amani yalitikiswa miaka miwili baadaye, mwezi Desemba 2013, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya serikali na makundi pinzani, hali iliyoendelea kuwaathiri mamilioni ya wananchi hadi leo.

    Katika juhudi za kurejesha amani, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, kwa ushirikiano na serikali ya jimbo la Equatoria Magharibi, umezindua kampeni mpya iitwayo "Tusikilizeni, Chukueni Hatua Sasa" (Hear Us, Act Now), inayolenga kuimarisha maridhiano, mshikamano wa kijamii na kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa amani. Feissal Kirwa, kupitia video ya UNMISS, amefuatilia uzinduzi wa kampeni hiyo na sasa anatuletea mada hii kwa kina.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili..

    1. Ripoti mpya ya hali ya saratani duniani kwa mwaka huu wa 2026 iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani (WHO) na shirika lake tanzu la utafiti wa saratani, IARC ikionya kuwa unyanyapaa ni moja ya vikwazo vya kutokomeza saratani wakati huu idadi ya wagonjwa ikikadiriwa kuongezeka maradufu ifikapo 2050, manusura wa saratani ya titi Abigael Hartz mkazi wa Ireland lakini anatokea Nigeria anasimulia alichoshuhudia alipotembelea hospitali moja ya kupima saratani Nigeria.
    2. Wiki mbili tangu matetemeko makubwa ya ardhi yapige mji mkuu wa Venezuela, Caracas na viunga vyake, idadi ya waliokufa imeripotiwa kufikia 3,685, majeruhi 16,740 na waliookolewa 6,462, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Msaada wa Dharura, OCHA, Tom Fletcher yuko nchini humo na anasema.. “Hapa ni La Guaira, ambalo kwa hakika ndilo eneo lililokumbwa zaidi na janga hili. Nimekutana na mama mmoja aliyepoteza watoto wake watano waliokuwa kwenye jengo lililo kule. Bado anasubiri kwa matumaini, ingawa matumaini hayo yanazidi kufifia, kwamba huenda watoto wake bado wakapatikana wakiwa hai. Kwa hiyo, tupo hapa katikati ya vifusi na harufu ya miili ya waliopoteza maisha, tukijitahidi kuwafikishia manusura chakula, maji na huduma za matibabu, huku tukiwasaidia kuanza kufikiria namna ya kujenga upya maisha yao. Lakini safari ya kurejea katika hali ya kawaida bado ni ndefu sana.”
    3. wakati huu ambapo ripoti za vyombo vya Habari zinaeleza kuwa jeshi la Marekani usiku wa kuamkia leo limekamilisha awamu mpya ya mashambulizi dhidi ya Iran, yakilenga zaidi ya maeneo 80 zikiwemo meli tatu za kibiashara zilizokuwa zinapita Mlango wa Bahari wa Hormuz huko Ghuba ya Uajemi, Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari, IMO Arsenio Dominguez amelaani mashambulizi hayo mapya akionya kuwa kwa mara nyingine maisha ya mabaharia wasio na hatia yanawekwa hatarini.
    4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KICHAKATA MATINI".

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!


    07 JULAI 2026 Jul 07, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili nampisha John Kibego wa redio washirika, Kazi Njema Redio nchini Uganda, kukueleza kuhusu harakati za kukuza lugha hiyo barani Afrika wakati huu ambapo UNESCO imeshaitangaza miaka mitano iliyopita kuwa lugha ya kimataifa.

    John, anamulika mpango wa ujenzi wa makao makuu ya kamisheni ya Kiswhaili ya Mungano wa Afrika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Ikiwa leo ni maadhimisho ya tano ya Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili chini ya Kaulimbiu "Kiswahili kwa Amani, Mshikamano na Diplomasia ya Uchumi wa Dunia" Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Togolani Mavura anafafanua ni kwa namna gani lugha ya Kiswahili inaweza kuyafanikisha hayo.
    2. Ugonjwa wa Ebola umeendelea kusambaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na idadi ya vifo vya watu imevuka 500 limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. Mwakilishi wa WHO nchini humo, Dkt. Anne Ancia akizungumza kwa njia ya video kutoka Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri mashariki mwa DRC ambako ni kitovu cha mlipuko huu, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kwamba kufikia tarehe 4 mwezi huu, serikali ya nchi hiyo ilikuwa imerekodi wagonjwa 1,561, vikiwemo vifo 506. Taarifa njema ni kuwa…“Jaribio la kitabibu lilianza tarehe 2 Julai kwa lengo la kubaini tiba madhubuti dhidi ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo.”
    3. Na asubuhi hii kwa saa za New York Marekani, kwa mara ya 34 tangu mwaka 1992, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekaa ili kujadili umuhimu wa kumaliza vikwazo vya kiuchumi na kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba tangu mwaka 1960. Katika barua ya mwaliko ambayo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amewapelekea wajumbe wa Baraza anasema, “ninayo heshima kukujulisha kwamba nimepokea barua iliyoambatanishwa ya tarehe 16 Juni 2026 kutoka kwa Mhe. Bwana Ernesto Soberón Guzmán, Mwakilishi wa Kudumu wa Cuba katika Umoja wa Mataifa, akiomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza Kuu ili kujadili ajenda namba 38 yenye kichwa: “Umuhimu wa kukomeshwa kwa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.”

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!


    06 JULAI 2026 Jul 06, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendelo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo limeendesha midahalo ya amani na utatuzi wa migogoro kwa vijana, lengo, ni kuimarisha amani kwa Maendeleo Endelevu.

    1. Siku nne tu baada ya shambulio kubwa la Urusi dhidi ya Ukraine, usiku wa kuamkia leo kwa saa za Ukraine wakazi wa Mji Mkuu, Kyiv kwa mara nyingine tena wamekumbana mashambulizi yaliyofanywa na Vikosi vya Wanajeshi wa Urusi. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Matthias Schmale, amesisitiza akisema, "haiwezi kurudiwa mara nyingi vya kutosha kwamba sheria za kimataifa za kibinadamu zinataka hatua zote zinazowezekana zichukuliwe ili kuwalinda raia na miundombinu ya kiraia." Mbali na mji mkuu, mwishoni mwa wiki mashambulizi ya mabomu katika mji wa Sumy yaliwaua raia kadhaa na kuwajeruhi makumi ya wengine, wakiwemo watoto. Miji mingine kama Dnipro, Kherson, Kyiv, Zaporizhzhia na mingine pia ilikumbwa na vifo na majeruhi wengi miongoni mwa raia pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kiraia, hali iliyokatiza upatikanaji wa huduma za msingi
    2. Hakuna dawa au mwanasesere anayefikia mtoto bila kufanyiwa kwanza uchunguzi au majaribio ya kina kuthibitishwa ni salama, lakini akili mnemba au AI imefikia watoto kupitia kusoma, urafiki au maswali binafsi ya msingi bila hata mtu mmoja kujiuliza athari mbaya za mfumo huo kwa watoto, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati wa ufunguzi wa Mjadala wa siku mbili kuhusu usimamizi wa akili mnemba ulioanza leo huko Geneva, Uswisi. Hivyo amesema, “hakuna mtoto anayepaswa kugeuzwa majaribio ya akili mnemba isiyodhibitiwa. Kwa kuendeleza kazi inayofanywa na Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na wadau wengine, leo ninatoa wito wa kupitishwa kwa Ahadi ya Usalama wa Watoto katika Matumizi ya akili mnemba, yenye kanuni tatu rahisi kwa mfumo wowote wa AI unaoweza kufikiwa na watoto.”.
    3. Na taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) iliyotolewa leo jijini London nchini Uingereza imemnukuu Katibu Mkuu wa shirika hilo, Arsenio Dominguez, akitoa wito wa hatua za haraka za kimataifa kuhakikisha mabaharia hao wanaachiliwa haraka na wakiwa salama. Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) iliyotolewa leo jijini London nchini Uingereza imemnukuu Katibu Mkuu wa shirika hilo, Arsenio Dominguez, akitoa wito wa hatua za haraka za kimataifa kuhakikisha mabaharia hao wanaachiliwa haraka na wakiwa salama

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!


    02 JULAI 2026 Jul 02, 2026
    Show notes

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tunaangazia fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo au kwa lugha ya kiingereza Internship hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Rashid Malekela kutoka Mwanza Tanzania, ambaye aliomba na kupata fursa hiyo anazungumzia na Leah Mushi wa Idhaa hii kueleza ni nini faida yake.

    1. Mashirika ya misaada nchini Ukraine leo Alhamisi Julai 2 yameongeza juhudi za kutoa msaada kufuatia ongezeko kubwa la mashambulizi makubwa yaliyofanywa na Urusi usiku wa jana, yakiwemo yale yaliyolenga mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kuwa miongoni mwa mashambulizi makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa dhidi ya mji huo.
    2. Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa zama za sasa Ashwini K.P ameonya kuwa ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni, ubaguzi dhidi ya jamii za pembezoni, na aina nyingine za kutovumiliana zinazohusiana na misingi hiyo bado vimejikita kwa kina katika ngazi zote za michezo duniani. Kwenye ripoti yake kwa Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu, mtaalamu amesema michezo ina uwezo wa kukuza ujumuishi, usawa na mshikamano wa kijamii, lakini bado inaendelea kuakisi na kuendeleza mifumo ya ubaguzi wa rangi na kimaeneo unaoshuhudiwa katika jamii kwa ujumla.
    3. Na huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania kumeanza mdahalo wa siku mbili wa vijana na amani ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na mmoja wa washiriki anatoa maoni.

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!


    Previous 1 12 13 14

    Related Podcasts

    How I Built This with Guy Raz

    1

    How I Built This with Guy Raz Business
    Planet Money

    2

    Planet Money Business
    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters

    3

    Inside Strategic Coach: Connecting Entrepreneurs With What Really Matters Business
    BiggerPockets Real Estate Podcast

    4

    BiggerPockets Real Estate Podcast Business
    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast

    5

    The Smart Passive Income Online Business and Blogging Podcast Business
    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn

    6

    A Thousand Natural Shocks With Gabe S. Dunn Business
    footer-logo

    Contact Us

    Toll Free: 844-670-7747

    Links

    • Home
    • Top Charts
    • Networks
    • Apps
    • Independents Podcasts
    • Podcast Advertising
    • Podcast News
    • Contact Us
    • About Us
    • Analytics & Insights

    Stay Connected

      Privacy, Terms of Use & Our Code of Ethics Protecting Content Creators Copyrights